Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dakta Zahar amesema kuwa, wananchi wote wa Palestina wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kusukuma mbele guruduumu la mpango wa kuikomboa Palestina kutoka katika makucha ya utawala ghasibu wa Israel.
Kiongozi huyo wa HAMAS ametaka kuainishwa malengo makuu ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO na kutupiliwa mbali makubaliano ya Oslo akibainisha kwamba, hii leo Ukingo wa Magharibi wa Mtojo Jordan unapaswa kufuata kigezo kinachofanyika katika Ukanda wa Gaza.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, viongozi mbalimbali wa makundi ya Palestina wameendelea kusisitiza kuwa, njia pekee ya kukabiliana na njama za Israel kama uporaji wa ardhi za Palestina ni kudumisha muqawama na mapambano dhidi ya maghasibu Wazayuni.
Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ulikuwa umepanga uanze kutekeleza siku ya Jumatano ya tarehe Mosi Julai mpango wake haramu wa kupora na kuunganisha asilimia 30 ya ardhi za Ufukwe wa Magharibi na ardhi zingine za Palestina unazozikalia kwa mabavu, lakini ukalazimika kuakhirisha na kusogeza mbele tarehe ya utekelezaji wake baada ya kushadidi mashinikizo ya upinzani ya Wapalestina na ya nchi mbali mbali duniani.
Mpango huo ni shemu ya mpango wa kibaguzi na uliojaa njama wa Muamla wa Karne unaopigiwa upatu na kuungwa mkono na serikali ya Rais Donald Trump wa Marekiani.
342/